Miaka Hamsini ya Kiswahili Nchini Kenya

This document was uploaded by one of our users. The uploader already confirmed that they had the permission to publish it. If you are author/publisher or own the copyright of this documents, please report to us by using this DMCA report form.

Simply click on the Download Book button.

Yes, Book downloads on Ebookily are 100% Free.

Sometimes the book is free on Amazon As well, so go ahead and hit "Search on Amazon"

Miaka Hamsini ya Kiswahili Nchini Kenya ni mkusanyiko wa makala yaliyowasilishwa katika kongamano la kimataifa la Kiswahili lililoandaliwa na Chama cha Kiswahili cha Taifa (CHAKITA) mwaka 2013, na likafanyika katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afrika Mashariki (CUEA). Makala chache zimetokana na kongamano la mwaka 2012 lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Kenyatta. Kitabu hiki kinadhihirisha umuhimu wa lugha ya Kiswahili katika nyanja mbalimbali za jamii. Kwa hiyo, utapata humu ndani makala yanayoangazia ufundishaji wa lugha ya Kiswahili; Kiswahili kama nyenzo ya maendeleo ya uchumi wa taifa; mchango wa Kiswahili katika kuleta uwiano na utangamano wa kitaifa; utafiti wa Kiswahili katika lugha na fasihi; Kiswahili na ujenzi wa taswira ya mwanamke; fasihi ya watoto katika Kiswahili; na athari za Sheng kwa Kiswahili. Kwa ufupi makala yaliyomo humu yanashadidia maendeleo ya Kiswahili katika miaka hamsini iliyopita nchini Kenya. Hiki ni kitabu muhimu sana kwa wanafunzi na walimu wa Kiswahili. Pia ni kitabu kitakachomnufaisha yeyote anayependa Kiswahili na anayetambua mchango wake katika jamii. Fifty Years of Kiswahili in Kenya is a collection of articles that were presented at an international Kiswahili conference organized by the National Kiswahili Association (CHAKITA) Kenya in 2013, which was held at the Catholic University of Eastern Africa (CUEA). A few articles are however from a similar conference held in 2012 at Kenyatta University. The book exemplifies the importance of the Kiswahili language in various sectors of society. Therefore, within this book you will find articles that focus on the teaching of the Kiswahili language; Kiswahili as a tool for national economic development; the contribution of Kiswahili to national cohesion and integration; Kiswahili research in language and literature; Kiswahili and portrayal of women; children’s literature in Kiswahili; and how Sheng affects Kiswahili. In short, the articles herein are a testimony of how Kiswahili has developed in the last fifty years in Kenya. This is a very important book for Kiswahili students and teachers. It is also an invaluable text for Kiswahili enthusiasts and all those who recognize its contribution to society.

Author(s): Inyani Simala; Leonard Chacha; Miriam Osore
Publisher: Twaweza Communications
Year: 2014

Language: Kiswahili (Swahili)
Pages: 288
City: Nairobi

Cover
Title page
Copyright page
Yaliyomo
DIBAJI
SHUKRANI
WAANDISHI WA MAKALA
UTANGULIZI
TUKIPENDE KISWAHILI
SEHEMU YA KWANZA - MIAKA HAMSINI YA LUGHA NCHINI KENYA
MIAKA HAMSINI YA UJENZI WA TASWIRA YA MWANAMKE KATIKA USHAIRI WA KISWAHILI NCHINI KENYA
MIAKA HAMSINI YA FASIHI YA WATOTO KATIKA KISWAHILI NCHINI KENYA: MAENDELEO NA CHANGAMOTO
KWA MIAKA HAMSINI, SHENG IMEKITUNZA KISWAHILI AU IMEKIUA?
SEHEMU YA pili - ufundishaji na ujifunzaji wa kiswahili
UFUNDISHAJI WA KISWAHILI UGHAIBUNI: MAENDELEO NA CHANGAMOTO
UFUNDISHAJI WA KISWAHILI SEKONDARI: NAFASI NA CHANGAMOTO ZA VITABU VYA KIADA
UFUNDISHAJI WA KISWAHILI KATIKA NCHI ZA KIGENI: MFANO WA CHUO KIKUU CHA SYRACUSE
CHANGAMOTO ZA KUJIFUNZA KIRAI NOMINO CHA KISWAHILI MIONGONI MWA WANAFUNZI: MCHANGO WA VITABU VYA KOZI VILIVYOIDHINISHA
SEHEMU YA TATU - kiswahili kama nyenzo ya maendeleo ya uchumi wa taifa
KISWAHILI KAMA LUGHA YA MAWASILIANO KATIKA SHUGHULI ZA BENKI: CHANGAMOTO ZA TAFSIRI
NAFASI YA KISWAHILI KATIKA UTEKELEZAJI WA RUWAZA 2030: TATHMINI YA KIPINDI CHA AWALI 2008 – 2012
SEHEMU YA NNE - KISWAHILI, UWIANO WA KITAIFA NA UTANGAMANO
DHIMA YA METHALI ZA KISWAHILI KATIKA KUELIMISHA JAMII KUHUSU UWIANO NA UTANGAMANO WA KITAIFA
MIZIKI YA KISWAHILI KAMA CHOMBO CHA KUHIMIZA UWAJIBIKAJI KATIKA JAMII: NYIMBO ZA MBARAKA MWARUKA MWINSHEHE
METHALI KAMA CHOMBO CHA KUSULUHISHA MIGOGORO YA KIJAMII
SEHEMU YA tano - utafiti wa kiswahili: lugha na fasihi
NAJIVUNIA KUWA MKENYA: UTOSARUFI, MTINDO AU MABADILIKO YA LUGHA?
JE SHENG NI LAHAJA YA KISWAHILI?: NADHARIA YA UTAMBULISHO WA LUGHA
TATHMINI YA TAFSIRI YA PENDEKEZO LA KATIBA YA KENYA 2010
TAFSIRI YA MAJINA YA PEKEE – UCHUNGUZI KIFANI WA MAJINA YA NCHI
LUGHA-ISHARA NCHINI KENYA: KATIBA NA MUSTAKABALI WAKE KISERA
UHAKIKI WA KITABU
Back cover