Historia ya Mapambano ya Mwafrika

This document was uploaded by one of our users. The uploader already confirmed that they had the permission to publish it. If you are author/publisher or own the copyright of this documents, please report to us by using this DMCA report form.

Simply click on the Download Book button.

Yes, Book downloads on Ebookily are 100% Free.

Sometimes the book is free on Amazon As well, so go ahead and hit "Search on Amazon"

Kwa karne kadhaa wakoloni na wabaguzi wa rangi wamekuwa wakieneza fikara mbaya kwamba “Waafrika hawakuwa na historia” mpaka watu kutoka nchi za mbali walipoingia na kufanya biashara nasi au kututawala. Kwa wakoloni maana ya “histona” ni matukio ya kale na ya sasa ya Ulaya au yanayowahusu Wazungu, binafsi au kitaifa. Wasomi wengi Waainmka kwanza waliikubali tafsari hii ya “historia”, wakaisoma, wakaitetea na kuieneza. Historia ya Tanzania, kwa mfano, kwao ingekuwa kwanza historia ya Waarabu kwenye pwani ya Afrika ya Mashariki mpaka kuingia kwa utawala wa Wajerumani na Waingereza. Mengineyo juu ya Tanzania yasingeitwa historia wacha kusomeshwa. Historia ya Mapambano ya Mwafrika kinachambua vizuri sana tatizo hili la “utovu wa historia ya Mwafrika” na hata kutupilia mbali maneno yaliyotumiwa kama vile “manegro, bushmen n.k.” ambayo yamejaa kasumba ya kashfa dhidi ya Waafrika. Lakini zaidi ya hayo kitabu hiki kina uchambuzi madhubuti wa kudhoofishwa kwa maendeleo ya kijamii — kiuchumi ya Waafrika na wageni na jinsi gani Waafrika wanaweza kujikomboa kikamilifu. Katika safu ya vitabu vya historia, Historia ya Mapambano ya Mwafrika ni kitabu cha lazima.

Author(s): H. Mapunda; D.N. Mwakawago
Edition: 3
Publisher: Tanzania Publishing House
Year: 1980

Language: Kiswahili (Swahili)
Pages: xvii,185
City: Dar es Salaam